H HALI TETE Mechi ya Mtibwa vs Simba | Uwanja Wageuka ‘Bwawa’ | Ndoo, Majaba Magodoro Vyatumika
Zikiwa Zimebak saa baki saa chache tu kuchezwa kwa mechi ya Ligi Kuu ya NBC itakayoikutanisha Mtibwa Sugar dhidi ya Simba SC katika uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro hali yaonekana si hali katika uwanja huo.
Ikumbukwe kwamba uwnaja wa Manungu ulifungiwa na Bodi ya Ligi kutumika katika mechi za Ligi Kuu na ni hivi majuzi tu ndio ulifunguliwa na kutumika
Sasa kwenye mitandao tayari zimesambaa video zikionesha hali ya uwanja huo ikiwa imejaa maji na juhudi za kuyaondoa zikiendelea kwa kutumia magodoro.
Hali hii ya uwanja oengine inaweza kuwa pigo lingine kwa Simba kwani mechi yao ya mwisho ya Ligi dhidi ya Mbeya City walikutana na changamoto hii kwenye uwanja wa Sokoine na kusababisha kupoteza mchezo huo kwa goli 1.
Sasa hali hii ya uwanja imewagusa mashabiki wengi na kuwafanya wahoji imekuwaje tena kwa uwanja kufunguliwa na kutumika ili hali miundombinu ya kutoa maji uwanjani haiko vyema.
Vipi, Mtibwa watatumia ubovu wa uwanja kama advantage na kuwafunga Simba au ni Simba watakaokuwa wakeanz akuzoea uwanja na kushusha kipigo kwa Mbeya City?
Weka maoni yako kwenye comment section hapo chini
...
https://www.youtube.com/watch?v=KsGnb2fIR8U