#UchaguziMkuu2020
BONYEZA LINK ? https://play.google.com/store/apps/details?id=com.habari.kwanza kudownload application ya Habari Kwanza sasa uwe wakwanza kupata habari, matukio na taarifa zote muhimu.
...
https://www.youtube.com/watch?v=JhT7iM83YYc
MAFINGA
AJALI YAUA 20 MAFINGA WENGINE 8 KUJERUHIWA.
Watu 20 wamefariki dunia na wengine 8 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea alfajiri ya leo Juni 10,2022 Mafinga Mjini eneo la Changarawe.
Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Scania yenye namba za Usajiri T 736 AAE na Coaster yenye namba za usajiri T542 DQV
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Mafinga Dkt.Victor Msafiri amethibitisha kupokea miili hiyo pamoja na majeruhi 8 na kwamba majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri huku miili ya watu 4 waliofariki ikiwa imetambuliwa na zoezi la utambuzi wa miili hiyo bado unaendelea.
Kufuatia kuripotiwa kwa habari hii, wananchi katika mtandao wa Twitter wametoa maoni mbalimbali ikiwemo ya kuitaka Serikali kuboresha miundombinu ya barabara za ‘highway’ kwa kuzitanua na kuzipa uwezo wa kupitisha gar 4 kwa wakati mmoja.
Lubasha Malili, kupitia Twiiter yeye amesema ifike muda sasa serikali iboreshe barabara za mikoani kwa kiziwekea njia 4 ili kuepusha ajali.
"Tukiweza hizi highways zetu zikawa 2/2 ajali za uso kwa uso tutapunguza nyingi." alikoment Lubasha
Naye Baba Assad CAG aliquote retweet na kusema kuwa mfumo wa one way umepitwa na wakati.
"Damu za ndugu zetu zinamwagika. Barabara ziendazo mikoani zijengwe katika mfumo wa Four ways, ziende gari mbili na kurudi mbili na ziwekewe partition kama kweli tunajali Uhai wa Watanzania.
mfumo wa one way umepitwa na wakati."
Mtazamaji wa Habari Kwanza, unadhani maoni ya Lubasha na JrMalcom88 yakifanyiwa kazi yataweza kupunguza ajali za barabarani zinazotokea katika barabara kuu? Ama wewe una maoni gani? Tunadikie kwenye comment section hapo chini….
#HabariKwanza
...
https://www.youtube.com/watch?v=xElJ6ZIUZtY
BONYEZA LINK ? https://play.google.com/store/apps/details?id=com.habari.kwanza kudownload application ya Habari Kwanza sasa uwe wakwanza kupata habari, matukio na taarifa zote muhimu.
...
https://www.youtube.com/watch?v=vE47WTYFkCE